Alhamisi , 3rd Aug , 2023

Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amefurahi ubora wa kikosi walichonacho katika kuelekea msimu mpya wa mashindano 2023/24 huku akiweka wazi malengo yao ni kuchukua mataji ya ndani.

Robertinho amesema kikosi chao  kina uwiano mzuri ambapo kwenye kila nafasi kuna wachezaji zaidi ya wawili wa kiwango cha juu.

Robertinho ameupongeza Uongozi wa klabu wa kusajili wachezaji bora huku akisema tumejipanga kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye michuano ya ndani pamoja na kimataifa.

“Nimeridhika na kambi ya maandalizi nchini Uturuki. Tumekuwa na wiki tatu nzuri huku tukiwa na kikosi bora pia. Tuna wachezaji zaidi ya wawili kwenye kila nafasi.

“Naupongeza Uongozi wa klabu kwa kufanya usajili huu mkubwa. Simba ni timu kubwa na tuna malengo ya kuchukua ubingwa wa ndani na kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa,” amesema Robertinho.