Mabingwa watetezi wa La Liga mara ya mwisho kupoteza mchezo wa ligi ilikuwa miezi 13 iliyopita na imecheza michezo 42 bila kupoteza, Barca inashakilia rekodi za kutokupoteza kwenye michezo 43 ya ligi iliyoanzia 2017 na 2018.Michezo mitatu iliyocheza Madrid dhidi ya Barcelona hivi karibuni kikosi cha Carlo Ancelotti kimeshinda michezo yote.
Kuelekea mchezo wa El Clasico utakaochezwa kesho Jumamosi Oktoba 26, 2024 rekodi zinaibeba Real Madrid mbele ya Wapinzani wao kutoka Jimbo la Catalunya FC Barcelona na timu hiyo Mabingwa watetezi wa ligi kuu Hispania inatarajiwa kuweka historia kwenye mchezo huo.
Mabingwa watetezi wa La Liga mara ya mwisho kupoteza mchezo wa ligi ilikuwa miezi 13 iliyopita na imecheza michezo 42 bila kupoteza, Barca inashakilia rekodi za kutokupoteza kwenye michezo 43 ya ligi iliyoanzia 2017 na 2018.Michezo mitatu iliyocheza Madrid dhidi ya Barcelona hivi karibuni kikosi cha Carlo Ancelotti kimeshinda michezo yote.
Barcelona inaongoza msimamo wa La Liga ikiwa imejikusanyia alama 27 katika michezo 10 iliyocheza imepoteza mchezo mmoja, Madrid inashika nafasi ya pili ikiwa na alama 24 baada ya kucheza michezo kumi ya ligi.
Kocha wa Barca raia wa Ujerumani Hansi Flick anategemea kikiosi chake chenye Vijana wengi wachanga wakiongozwa na Raphinha, Lmine Yamal, Pedri na Fermin Lopez wakisaidiwa na mkongwe Robert Lewandoski wanatarajia kuonyesha upinzani mkubwa siku ya kesho Jijini Madrid.
Nyota wawili kutoka Brazil wanatizamiwa kuonyesha viwango bora kesho uwanjani Santiago Bernabeu Vinicius Junior na Raphinha aliye kwenye kiwango bora chini ya Hansi Flick amehusika kwenye goli 17 msimu huu akiwa amefunga goli 9 na upatikanaji wa mengine 8. Alifunga hat-trick dhidi ya Bayern Munich kwenye mchezo uliochezwa siku ya Jumatano wa ligi ya Mabingwa barani Ulaya.
Vinicius JR anapigiwa chapuo na Wadau wengi wa soka Duniani kushinda tuzo ya mchezaji bora Duniani kutokana na muendelezo wa kiwango bora anachokionyesha ndani ya Madrid tangu msimu uliopita. Alifunga goli tatu hat-trick kwenye mchezo wa ligi ya Mabingwa Ulaya siku ya Jumanne dhidi ya Borrusia Dortmund ya Ujerumani.
Real Madrid na Barcelona zitakutana kesho Jumamosi kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu katika mchezo wa La Liga huku timu zote zikiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi ulioupata Katikati ya wiki ambapo Madrid ilishinda 5-2 dhidi ya Borrusia Dortmund huku Barca ikiichapa Bayen Munich 4-1 uwanja wa Camp Nou.