
Bosi wa klabu ya PSG, Nasser El Khelaif (Kushoto) akimkabidhi Neymar Jr (Kulia) mara baada ya kukamilisha usajili wa nyota huyo raia wa Brazil.
Katika misimu yake mitatu aliyoitumikia miamba hiyo ya Ufaransa, Neymar amekua na mchango mkubwa ambapo amecheza michezo 82 na kuifungia mabao 70.
Pia ameisaidia PSG kushinda mataji ya ligi kuu ya Ufaransa kwa misimu yote tangu ajiunge na klabu hiyo na pia hivi sasa wapo robo fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya.
Hivi sasa ni miaka mitatu imetimia tangu mshambuliaji huyo wa Brazil atue PSG, huenda akaipa mafanikio makubwa ya Ulaya msimu huu.