
Hayo yamethibitishwa mnamo Novemba 19,2023 na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa katika mapokezi ya timu ya Taifa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ambapo ametumia nafasi hiyo kusema kuwa Stars itaishangaza Dunia kwa kuifunga Morocco huku akiwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Benjamin Mkapa Novemba 21,2023.