Jumatano , 29th Oct , 2014

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba ya jijini Dar es salaam, Ismail Aden Rage amemtaka Rais wa sasa wa Klabu hiyo Evance Aveva kukutana na wanachama waliofukuzwa katika klabu hiyo ili kuweza kumaliza tofauti zao.

Akizungumza na East Africa Radio, Rage amesema iwapo Aveva atakubali kumaliza migogoro iliyopo katika klabu hiyo, itasaidia kuleta maendeleo ya Klabu na hata migogoro midogo midogo iliyopo hivi sasa itamalizika.

Rage amesema katika migogoro inayoendelea hivi sasa, wanachama wa klabu hiyo wanatakiwa kuwa wavumilivu kutokana na matokeo yaliyopo hivi sasa na anaamini mkutano mkuu unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni utakuwa ni suluhisho la matatizo yaliyopo katika klabu hiyo.