Alhamisi , 2nd Nov , 2023

Shirikisho la soka nchini Uganda (FUFA) limemtambulisha kocha Paul Put raia wa Ubelgiji kuwa kocha mpya wa timu ya Taifa Uganda 'The Cranes' kwa mkataba wa miaka miwili.

Put  mwenye umri wa miaka 67 anachukua nafasi ya Milutin Sredojevic 'Micho' aliyefutwa kazi mwezi Septemba mwaka huu. Kocha huyo ana uzoefu wa soka la Afrika amewahi kuzinoa timun za mataifa ya Gambia, Burkina Faso, Gabon, Kenya, Guinea na Congo kwa nyakati tofauti.