Jumamosi , 8th Mar , 2014

Makocha watatu toka vikundi vitatu waendesha mafunzo yakuendeleza vijana

Mpango maalumu wa kukuza na kuendeleza vijana wa dogo katika mchezo wa mpira wa kikapu nchini ujulikanao kama Basketball Across Borders umeendelea hii leo katika viwanja vya shule ya kimataifa ya Tanganyika IST Masaki jijini Dar es salaam

Kocha mkuu wa vijana hao Bahati Mgunda amesema kuwa mpango huo ulianza na wachezaji 68 na baada ya mchuajo wa kwanza wamebaki 14 ambao wanaendela na mafunzo na baadae watachujwa na kubaki 10 ambao wataenda katika mashindano kule Quebec Canada

katika hatua nyingine baadhi ya wachezaji ambao wako katika mpango huo Jeska James na Janush Kompany wamefurahishwa na mpango huo na wamesema kuwa wanataraji mpango huo utawasaidia kufika mbali japo ushindani ni mkubwa.