Jumatatu , 19th Oct , 2020

Mlinzi wa Liverpool Virgil van Dijk atafanyiwa upasuaji wa goti baada ya kupata majeruhi kwenye mchezo dhidi ya mahasimu wao Everton kwenye mchezo wa ligi kuu EPL, ambao ulimalizika kwa sare ya magoli 2-2.

Mlinzi wa Liverpool Virgil Van Dijk alipokumbana na mlinda mlango wa Everton, Jordan Pickford ambapo baada ya kugongana nae aliondolewa uwanjani.

Inakadiriwa Van Dijk anaweza kukaa nje ya uwanja kwa muda wa miezi 8 kutokana na ukubwa wa jeraha hilo, huku tukiwa bado tunasubiri taarifa rasmi juu ya muda atakao kosekana.

Kukosekana kwa beki huyo wa kimataifa wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 29, litakuwa pengo kubwa kwa kocha Jurgen Klopp kwani tangu Virgil van Dijk ajiunge na Liverpool amekuwa mwarobaini wa matatizo kwenye safu ya ulinzi ya kikosi hicho.

VVD alijiunga na mabingwa hao wa England January 2018 akitokea Southampton kwa ada ya uhamisho ambayo ilikuwa ni rekodi ya Dunia kwa beki kwa kipindi hicho, Pauni milioni 75 ambayo ni zaidi ya Bilioni 226 kwa pesa za kitanzania.

Takwimu zinaonyesha tangu Van Dijk ajiunge na Liverpool amekosa mchezo mmoja tu wa ligi kuu, na ameisaidia timu yake kushinda jumla ya alama 196, zikiwemo alama 97 za msimu wa 2018-19 ambao walimaliza nafasi ya pili, na alama 99 msimu wa 2019-20 ambao walichukua ubingwa wa EPL.

Ni Aymeric Laporte na Kyle Walker wa Manchester City ndio mabeki wenye wastani mzuri wa kutoruhusu goli kwa dakika zaidi wa VVD.

Aymeric Laporte ana wastani wa kuruhusu goli kila baada ya dakika 158, Walker kila baada ya dakika 120 na Van Dijk wastani wake wa kuruhusu ni kila baada ya dakika 111.

Lakini pia katika michezo 95 ya ligi kuu kuu aliyocheza mlinzi huyo, Liverpool wamefungwa mabao 78 na hawajaruhusu goli katika michezo 44.

Wastani wa Liverpool kuturuhusu goli ulikuwa mkubwa kabla ya VVD kujiunga na majogoo ambapo waliruhusu mabao 117 katika ichezo 95 na ni katika michezo 29 tu ndio ambayo hawakurushusu goli.

Katika ufungaji pia Van Dijk amekuwa bora miongoni mwa mabeki anashika nafasi ya pili katika orodha ya mabeki waliofunga mabao mengi tanga beki huyo ajiunge na Liverpool amefunga jumla ya mabao 10 akizidiwa na Patrick Van Aanholt wa Crystal Palace.

Anashika nafasi ya pili kwenye wastani bora wa kushinda mipira ya juu akizidiwa na mchezaji mwenzake wa Liverpool, Joel kwa wastani wa asilimia 75.7% za Matip nayeye ana asilimia 74.6%, japokuwa VVD amepambania mipira ya juu mara nyingi zaidi  (622)na Matip  (173).

Kwa takwimu hizi za VVD, Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp anahitaji kupata mlizni mwenye sifa za kubeba majukumu kikamilifu kama ilviyokua kwa mholanzi huyo ambaye amedhihirisha ubora wake katika misimu miwili na nusu aliyodumu Anfield.

Walinzi wa kati waliosalia kikosini ni Joel Matip, Joe Gomes ambao kwa wastani wamezidiwa kwa takwimu na Van Dijk.