Jumamosi , 14th Aug , 2021

Paul Pogba amevunja rekodi ya Lionel Messi aliyoiweka mwezi Aprili 29, 2012 wakati klabu yake ya zamani Barcelona ilipokuwa ikipepetana na Rayo Vallecano ambapo alitoa pasi za mwisho (assist) 3 zilizozalisha magoli kwenye ushindi wa goli 7 bila.

Picha ya Pamoja wachezaji Paul Pogba na Bruno Fernandes

Pogba ametoa pasi za mwisho (assist) 4 zilizozalisha magoli katika ushindi wa goli 5-1 wakati Manchester United ilipo wakaribisha Old Trafford kwenye mchezo wa pili wa ligi kuu England (Premier League) Leeds United.