Alhamisi , 24th Sep , 2020

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amesema kwasasa itakuwa ngumu kwa kiungo wake wa kijerumani, Mesut Ozil kuanza katika kikosi cha kwanza kwani ushindani umekuwa mkubwa sana katika timu hiyo jambo linalopelekea kumnyima namba nyota huyo.

Mesust Ozil akiwa kwenye taswira ya huzuni akiwa anaondolewa uwanjani.

Ozil hakuwepo katika kikosi kwenye mechi nne za mwanzo wa msimu huu ambazo washika mitutu hao walipata matokeo mazuri.

Miongoni mwa michezo hiyo, ni miwili ya ligi kuu, mmoja wa kombe la Carabao walioshinda 2-0 dhidi ya Leicester kwenye uwanja wa King Power.

Ikumbukwe pia Arsenal waliifunga Liverpool kwa changamoto ya mikwaju ya penati katika mchezo wa ngao ya hisani uliopigwa Agosti mwaka huu, bila kiungo wao Mesut Ozil.

"Kwasasa timu inabadilika sana kama unavyoona imefikia katika hatua ya mafanikio”Alisema Arteta, .

"Hapa ndipo tulipokuwa kwasasa, tunataka tubadilike sana, tucheze vizuri na tushindane, lakini pia nina furaha na kiwango wanachokionesha wachezaji wangu na inanipa ugumu kuchagua wachezaji wakuanza.

Tunachagua wachezaji ambao tunaamini ni bora katika kila mchezo, kama unavyoona tunaendelea na mazoezi, hivi ndiyo tunavyofanya.” Aliongezea Mikel.

Ozil mwenye miaka 31 hajacheza mchezo wowote tangu kurejea tena kwa msimu wa 2019/20 mwezi juni huku mechi yake ya mwisho ikiwa ni Machi 7.

Ozil akiwa Arsenal amecheza mechi 184 za ligi kuu ya England, amefunga magoli 33 na kuhusika kwenye ushindi katika mechi 100, pia amepiga pasi 11,186 na kutengeneza nafasi 54 za mabao kwenye ligi hiyo.