Awali Onana alikubali kurejea katika kikosi cha timu hiyo ya taifa kwa ajili ya mchezo mmoja tu pekee ambao walicheza dhidi ya timu ya taifa ya Burundi, na baada ya hapo akasema kuwa kutakuwa na mazungumzo zaidi ikiwa watafuzu AFCON, na hivi sasa wameshafuzu na hivyo amekubali kurejea tena.
Jumatano , 1st Nov , 2023
Mlinda mlango wa Manchester United André Onana amekubali kuichezea Cameroon kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON mwezi Januari, na hivyo kutokana na maamuzi hayo anaweza kukosa mechi saba za nyumbani ambazo Man U watacheza.