
Emmanuel Okwi
Kocha Mubiru, amemtangaza mchezaji mzoefu kikosini Emmanuel Okwi anayecheza Al Ittihad Alexandra ya Misri kuwa nahodha wa kikosi katika mchezo huo, ikumbukwe kuwa nahodha mkuu wa timu hiyo Denis Onyango alitangaza kustaafu siku chache zilizopita baada ya kuitumikia timu ya taifa kwa zaidi ya miaka 15
Katika kikosi hicho wapo pia wachezaji wanaocheza ligi kuu Tanzania bara waliojumuishwa akiwemo kiungo mkabaji wa Simba Taddeo Lwanga, pamoja na kipa wa Azam Mathias Kigonya, huku Nicolaus Wadada akiachwa pamoja na uzoefu wake .
Kwa mujibu wa kocha huyo, timu itaingia kambini asubuhi saa 2:00 siku ya jumapili tarehe 30/5/2021 na mazoezi rasmi yataanza jumatatu katika uwanja wa MTN Lugogo.
Mechi hii ya kimataifa ya kirafiki ni sehemu za maandalizi pia ya mechi za kufuzu kwa kombe la dunia zitakazoanza baadaye m mwaka huu, Uganda imepangwa kwenye kundi E na Mali, Rwanda na Kenya.