
Katika taarifa yake, meneja wa African Sports, Abdul Bosnia amesema, wamemsajili Nsa Job ili kuimarisha kikosi chao na wana imani atawasaidia ikizingatiwa kwamba ni mchezaji mzoefu hivyo kwa kushirikiana na wachezaji wengine waliopo watafanya vizuri.
Job ambaye amewahi kukipiga Villa Squad, Yanga na Simba kwa muda mrefu alikuwa nje ya dimba baada kuvunjika mguu wakati akiichezea Coastal Union mechi ya ligi kuu dhidi ya JKT Ruvu.