Jumatatu , 10th Dec , 2018

Timu ya taifa ya Tanzania ya soka la ufukweni leo inakabiliwa na kibarua kigumu dhidi ya Nigeria katika mchezo ambao utaamua hatma ya timu hiyo kwenye kundi B la michuano ya AFCON inayoendelea nchini Misri.

Wachezaji wa timu ya taifa ya Nigeria inayoshiriki AFCON ya soka la ufukweni nchini Misri.

Tanzania tayari imeshapoteza mechi zake mbili za kwanza katika kundi hilo, ikifungwa 5-2 na Libya kwenye mchezo wa kwanza kisha jana kupoteza kwa mabao 12-2 dhidi ya Senegal.

Kundi hilo sasa linaongozwa na Senegal ambao walishinda mechi zao mbili za kwanza, wakianza na Nigeria walipowafungwa kwa penati 2-0 baada ya kutoka sare ya 4-4 kwenye muda wa kawaida.

Wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania inayoshiriki AFCON ya soka la ufukweni nchini Misri.

Libya wapo nafasi ya pili wakiwa wameshinda mechi moja dhidi ya Tanzania kwa mabao 5-2 huku Nigeria wakiwa nafasi ya tatu baada ya kushinda mechi yao dhidi ya Libya kwa mabao Libya 3-6 Nigeria.

Tanzania leo inatakiwa kushinda kwa idadi kubwa ya magoli kisha kuomba Senegal waifunge Libya kisha idadi ya mabao ya kufunga na kufunga yaamue kati ya timu ya taifa ya Tanzania na Libya ambayo itaungana na Senegal.