Kwa mujibu wa msemaji huyo wa zamani wa Yanga amesema kuwa ametekeleza faini aliyopaswa kuilipa kunako Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini na tayari ameziwasilisha TFF na amegongewa mhuri wa risiti zake.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Manara amesema anakwenda kushirikiana na idara ya habari ya Yanga kuitetea nembo ya Yanga na hatovumilia kuona mtu anaichafua nembo hiyo akitamba kuwa hajawahi kuwa mnyonge kwenye jambo hilo.
Ikumbukwe Manara alifungiwa kujihusisha na shughuli za mpira wa miguu kwa kipindi cha miaka miwili ambapo kwa mujibu wake ameeleza kuwa amemaliza adhabu hiyo.