Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Ngorongoro Heroes kusuka au kunyoa leo, AFCON U20

Jumatatu , 22nd Feb , 2021

Timu ya taifa ya Tanzania chini ya miaka 20 'Ngorongoro Heroes', saa 4:00 usiku wa leo Februari 22,  2021 inataraji kushuka dimbani kucheza dhidi ya Morocco U20 kwenye mchezo wa mwisho kundi C kuwania nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya AFCON U20 nchini Mauriatania.

Wachezaji wa Ngorongoro Heroes wakifanya mazoezi ya mwisho kabla ya kuwavaa Morocco leo.

Kuelekea kwenye mchezo huo ambao Ngorongoro Heroes wanahitaji ushindi ili kuweka hai matumaini ya kutinga hatua hiyo, Nahodha wa timu hiyo Kelvin John amesema wanaamini watafuzu kutokana na walivyojipanga  kwenda  kupata matokeo mazuri.

“Tunajua Morocco ni timu nzuri na sisi tumejipanga kwenda kupata matokeo kwenye mchezo huo, bado tuna nafasi kubwa ya kuweza kupata matokeo kwahiyo, kikubwa zaidi tunapokea maelekezo vizuri kutoka kwa mwalimu wetu na mipango yake ili tuweze kufanya vizuri kwenye mchezo  huo”.

Kwa upande wa kocha wa kikosi hicho, Jamhuri Kihwelo 'Julio', amesema “Tunakutana na Morocco, hatuogopi ushindani huu uliopo kwa wenzetu waliotangulia kabla yetu, lakini tunasema tu, kubwa tunataka tushinde ili tupate nafasi ya kuendelea”.

Ngorongoro Heroes ikipata ushindi, itafikisha jumla ya alama 4 na kuombea mchezo wa Gambia dhidi ya Ghana utakaochezwa muda mmoja umalizike kwa sare ili wamalize nafasi ya tatu na kufuzu kwakuwa 'Best loser' kwani Tunisia kutoka kundi B imefuzu ikiwa best loser kwa kuwa na alama 4.

Kundi A, wenyeji Mauritania wameshika nafasi ya tatu wakiwa na alama 3 hivyo wataweza kufuzu hatua ya robo fainali endapo Ngorongoro Heroes na Gambia kutoka kundi C watafungwa ama kutoka sare na wawili hao kusalia na alama  mbili mbili.

Timu tano zilizofuzu kucheza hatua ya robo fainali ni, vinara wa kundi A, Cameroon, Uganda walioamliza wapili, Kundi B, Burkina Faso, Central Afrika na Tunisia ikiwa ni 'Best loser'.

Hatua ya robo fainali ya michuano hii ambayo Ngorongoro Heroes wanashiriki kwa mara ya kwanza, inatazamiwa kuchezwa siku ya Alhamisi ya tarehe 25 Februari 2021 nchini Mauritania ambao ndiye wenyeji wa michuano hiyo.

HABARI ZAIDI

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine

Kaimu Mkurugenzi wa ufuatiliaji na uzingatiaji sheria NEMC,

Wamiliki wa Hospitali nchini wapewa siku 90

Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Madanga Mkoani Tanga

Wagoma kubeba mimba kwa kukosa huduma za afya