Mbwana Samatta
Ni baada ya droo ya hatua ya makundi ya Klabu Bingwa barani Ulaya kufanyika usiku wa jana, ambapo timu ya mshambuliaji huyo (KRC Genk) imepangwa katika kundi E pamoja na timu za Liverpool, Napoli na RB Salzburg.
Moja katika ndoto ya Samatta ni kucheza Ligi Kuu nchini Uingereza EPL, ambapo katika moja ya kauli zake aliwahi kusema, "siku zote toka nikiwa mtoto tulikuwa tunaenda kwenye mabanda ya kuonesha mpira na nilikuwa napenda kuangalia EPL, ni kitu ambacho kinanivutia sana. Napenda kucheza ligi ya Uingereza lakini huwezi jua itakuwaje".
Kwa namna moja ama nyingine Samatta atakuwa ametimiza ndoto ya kucheza na moja ya timu kubwa inayoshiriki EPL, ambao ni mabingwa watetezi wa Klabu Bingwa Ulaya, Liverpool. Itakuwa ni mara ya kwanza kwake kucheza Uingereza.
Rekodi nyingine ambayo ataiweka Samatta katika michuano hiyo ni kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza Klabu Bingwa Ulaya na mchezaji wa tatu wa Afrika Mashariki kucheza michuano hiyo baada ya McDonald Mariga na Victor Wanyama, wote raia wa Kenya.

