
Katibu Mkuu wa Ndanda Selemani Kachele amesema, wamepanga kuongeza wachezaji saba ili kuimarisha kikosi chao kiweze kupambana ipasavyo.
Kachele amesema, wamekiangalia kwa umakini kikosi na kugundua kuwa kuna baadhi ya mapungufu na kugundua kuwqa kati ya wachezaji hao wanahitajika mabeki wawili, viungo watatu, straika mmoja na kipa mmoja ili kuwa kujiweka vizuri kwa msimu ujao.
Ndanda haikuwa na msimu mzuri katika msimu uliopita, na ililazimika kufanya kazi ya ziada ili kubaki Ligi Kuu Bara.