Jumatano , 17th Jun , 2015

Mshambuliaji mkongwe Gaudence Mwaikimba ametua JKT Ruvu iliyopania kujiimarisha ili ifanye vizuri msimu ujao wa ligi kuu soka Tanzania Bara.

Mwaikimba aliyekuwa akikipiga Azam FC, amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea JKT Ruvu huku timu hiyo ikiwa tayari JKT imefanikiwa kumsainisha mshambuliaji Saad Kipanga kutoka Mbeya City.

Katika taarifa yake Makamu Mwenyekiti wa JKT Ruvu Meja Hassan Mabena amesema usajili wanaoufanya una lengo la kujiimarisha kwa ajili ya msimu ujao na hawajaishia hapo, wanaendelea kusajili vifaa zaidi.