Jumanne , 25th Mar , 2014

Mabondia watanzania Tomas Mashali na Japhet kaseba wako katika maandalizi ya mwisho mwisho wakijiwinda na mpambano wao wa kimataifa kuwania ubingwa wa UBO utakaopigwa mwishoni mwa mwezi huu jijini Dar es salaam

Mratibu wa Pambano hilo Musa Kova amesema kuwa kila kitu kimekamilika ambapo bondia mrusi na kundi lake watawasili aprili mosi huku Chaka ambaye yuko jijini Nairobi Kenya akijifua akitaraji kurejea nchini march 28 tayari kuhakikisha anaubakisha mkanda huo wa UBO kilo 81 katika pambano la raundi 10

Aidha Kova amesema kila kitu kwa wao kama waandaaji kimekamilika na hivyo amewataka watanzania kuunga mkono juhudi hizo za mapromota ambao wanawaletea mabondia wa hapa nchini mapambano makubwa.