Bondia Mtanzania, Twaha Kiduku (wa kwanza kushoto) akipima uzito kwa matayarisho ya moja ya pambano lake.
Akizngumza na East Africa Radio, Katibu wa shirikisho la masumbwi PST, Antony Lutha amesema kwamba matayarisho kuelekea pambano hilo la Oktoba 30 mwaka huu yamekamilika kwa kiasi kikubwa.
Pambano hilo linatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa PTA huku waamuzi watakaoamua pigano hilo wakitajwa kuwa ni Filermon Mweya kutoka Namibia, Mtanzania John Chagu na Ms Lynette Onam wa Kenya huku Irene Semaya toka Uganda akitajwa ndiye msimamizi mkuu wa pambano hilo.
Rekodi inaonesha mthailand, Sirimongkhon lumthuan amecheza mapambano 101 huku akipigwa mechi 4 tu na kwa upande wa Kiduku kapanda ulingoni mara 22 na kapigwa mechi 6 na droo mara 1.