Mourinho awapinga mashabiki

Tuesday , 5th Dec , 2017

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amekwenda tofauti na mashabiki wa soka kwa kusema, golikipa namba moja wa klabu hiyo David De Gea anashika namba tatu kwa ubora duniani.

Akiongea na wanahabari kwenye mkutano kuelekea mchezo wa UEFA leo ambapo Manchester United itaikaribisha CSKA Moscow, Mourinho amesema golikipa namba moja duniani ni Sergio Romelo ambaye ni golikipa namba mbili kwenye kikosi chake.

Alipoulizwa iwapo amewahi kufanya kazi na mlinda mlango bora zaidi ya De Gea Mournho amejibu, “Ndio, Sergio Romelo, kwasababu atacheza dhidi ya CSKA Moscow, magolikipa wangu wote huwa ni bora duniani”.

Mourinho ameongeza kuwa kwasasa golikipa namba mbili duniani ni Joel Castro Pereira ambaye ni golikipa namba tatu kwenye kikosi cha Man United wakati David De Gea anashika nafasi ya tatu kwa ubora duniani.

Kocha huyo Mreno amekuwa tofauti na mashabiki wengi wa soka duniani ambao hivi karibuni wamekuwa wakimtaja De Gea kama golikipa namba moja duniani kutokana na uwezo wake alioonesha kwenye mchezo dhidi ya Arsenal wikiendi iliyopita.