Jumapili , 1st Nov , 2020

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya klabu ya soka ya Simba, Mohammed Dewji, amesema mpira wa Tanzania kamwe hautasonga mbele kutokana na mwenendo wa uchezeshaji.

Mohammed Dewji

Mo Dewji ametoa malalamiko hayo kupitia kurasa zake za mkitandao ya kijamii, akitolea mfano goli la Luis Miquissone dhidi ya Mwadui FC, lililokataliwa kuwa ni la kuotea.

Waamuzi wa Tanzania wamekuwa wakilalamikiwa juu ya uchezaji wao hususani kwenye maamuzi yenye utata kama ya kuotea na matukio ya katikati ya uwanja.

Hivi karibuni Shirikisho la soka Tanzania kupitia Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu soka Tanzania bara ilimfungia mwamuzi Shomari Lawi miezi 12 kutojihusisha na soka kutokana na makosa mbalimbali katika kazi yake.