Ijumaa , 4th Nov , 2016

Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa ametaja kikosi cha wachezaji 24 kitakachoingia kambini Novemba saba kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Zimbabwe utakaopigwa Novemba 13 mwaka huu nchini humo.

Boniface Mkwasa - Kocha wa Taifa Stars

Nyota wa Stars walioitwa na Mkwasa ni:

Makipa

Deogratius Munishi             –Young Africans

Said Kipao                        –JKT Ruvu

Aishi Manula                     –Azam FC

 

Mabeki

Erasto Nyoni                     -Azam FC

Michael Aidan                    -JKT Ruvu 

Mwinyi Haji                      -Young Africans

Mohamed Hussein              –Simba SC

David Mwantika                 -Azam FC

James Josephat                 –Tanzania Prisons

Vicent Andrew                   -Young Africans

 

Viungo wa Kati

Himid Mao                        -Azam FC

Mohammed Ibrahim            –Simba SC

Jonas Mkude                     –Simba SC

Muzamiru Yassin                –Simba SC

 

Viungo wa Pembeni

Abdulrahman Mussa            -Ruvu Shooting         

Shiza Kichuy                      –Simba SC

Simon Msuva                     -Young Africans

Jamal Mnyate                    –Simba

 

Washambuliaji

Ibrahim Ajib                      –Simba SC

John Bocco                        -Azam FC

Mbwana Samatta                -K.R.C Genk ya Ubelgiji

Elius Maguli                       –Oman

Thomas Ulimwengu            –Mchezaji huru

Omar Mponda                    -Ndanda

Kwa sababu mbalimbali hususani majeruhi, Mkwasa amewaacha wachezaji Shomari Kapombe (Azam FC), Hassan Kabunda (Mwadui FC), Juma Abdul na Juma Mahadhi wa Young Africans.

Mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika jijini Harare, umeratibiwa kwa mujibu wa kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambalo huwa na kalenda ya wiki ya mechi za kimataifa kwa wanachama wake – Tanzania ni miongoni mwao. Shirikisho la Mpira wa Miguu la Zimbamwe liliomba TFF mchezo huo.

Matokeo ya mchezo huo, ni sehemu malumu kupima viwango vya ubora na uwezo wa timu za taifa. Kwa sasa Tanzania inashika nafasi ya 144 kati ya nchi 205 wanachama wa FIFA zilizopimwa ubora. Zimbambwe yenyewe inashika nafasi ya 110.