Ijumaa , 30th Jan , 2015

Mkutano Mkuu wa Klabu ya Simba uliokuwa ukitarajiwa kufanyika Januari 11 mwaka huu unatarajiwa kufanyika Machi Mosi mwaka huu ukiwa na lengo la kujadili mambo mbalimbali yatakayosaidia kukuza na kuboresha klabu hiyo.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Rais wa Klabu hiyo, Evance Aveva amesema, walipanga kufanya mkutano huo kama walivyopanga lakini waliahirisha kutokana na muingiliano wa Ratiba ambapo Timu ya Simba ilikuwa visiwani anzibar kushiriki Michuano ya Kombe la Mpinduzi.

Aveva amesema, wamewasiliana na wanachama wa klabu hiyo, ambao wanatarajia kukutana tarehe rasmi waliyopanga sasa ambapo kutakuwa na mambo mbalimbali yatakayojadiliwa kuhusu klabu hiyoa mabyo anaamini yatazidi kukuza klabu.

Kwa upande mwingine Aveva amewataka mashabiki wa klabu hiyo kuwa wavumilivu katika kipindi hiki wakati timu ikirekebisha makosa yanayochangia timu hiyo kuweza kufanya vibaya katika Michuano ya Ligi kuu Tanzania Bara.

Aveva amesema, suala kubwa linalochangia timu hiyo kuwa katika nafasi mbaya ni jinsi mpangilio wa ratiba ulivyokaa ambapo timu inacheza mechi za karibu karibu ambazo ni za viporo kutokana na kushindwa kushiriki mechi hizo wakati wapo katika michuano ya kombe la mapinduzi.