
Moja ya mchezo wa kikapu
Kamishna wa Ufundi wa Mashindano wa Chama Cha Mpira wa Kikapu nchini TBF Manase Zabron amesema mpaka sasa ni mikoa 25 iliyohakiki ushiriki na kwa upande wa chama wameshajiandaa kwa ajili ya mashindano pamoja na Mkutano Mkuu ambao ndani yake kutakuwa na upangaji wa ratiba utakaofanyika Novemba 30 mwaka huu jijini Arusha.
Manase amesema timu zote shiriki zinaendelea na maandalizi na wanaamini watapata timu bora ya taifa itakayoiwakilisha nchi katika mashindano mbalimbali ya kimataifa.
Mashindano ya Taifa Cup yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Desemba Mosi mpaka 10 mwaka huu jijini Arusha.