Shirikisho la ngumi za kulipwa Tanzania PST hii leo limepokea mikanda miwili ya ubingwa wa kimataifa na wa dunia kwa bara la afrika iliyoagizwa toka nchini Denmark
Katibu mkuu wa PST Anthony Rutta amesema kuwa kuwasili kwa miakanda hiyo miwili ni kiashirio cha kukamilika kwa maandalizi ya mapambano makubwa mawili yatakayopigwa march 29 mwaka huu katika ukumbi wa PTA jijini Dar es salaam
Ambapo mpambano mkubwa main card ni kati ya mabondia Thomas Mashali atakayevaana na Japhet Kaseba
Rutta amesema tayari kwa asilimia 95 kila kitu kimekamilika kwa mapambano hayo na hivyo kuwataka mabondia wote watakaopanda ulingoni siku hiyo waendelee na maandalizi mazito na kujipanga kutoa burudani kwa mashabiki watakaofika kutazama mapambano yote siku hiyo.