Wawakilishi hao wataenda kuiwakilisha Tanzania, katika michuano ya jumuiya ya madola itakayofanyika jijini Grascow Scotland.
Katibu mkuu wa JATA Innocent Malya, amesema kuwa baada ya maafikiano sasa kila kitu kiko sawa na wamekubaliana watumie mashindano ya Afrika Mashariki kupata wawakilishi wa pande zote, kwa sifa ile ile ya mshindi wa medali ya dhahabu ndiye atakayefuzu kuwakilisha nchi katika michuano hiyo.
