Jumatano , 24th Sep , 2014

Kocha wa mchezo wa Riadha kwa vijana Said Muhunzi amesema kozi anayoendelea nayo kwa vijana hao wenye Umri wa miaka 12 kutoka shule mbalimbali mkoani Dar es salaam itasaidia kukuza mchezo huo hapa nchini.

Wanariadha watoto

Akizungumza na Muhtasari wa michezo Muhunzi amesema ili kuweza kukuza michezo hapa nchini inahitajika kuanzia kwa vijana ili kuweza kufanikisha ukuzaji wa michezo.

Aidha Muhunzi amesema ili kuwapa mafunzo yatakayowapa uelewa wa michezo inahitajika muda wa kukaa nao ili kuwaendeleza kwa ajili ya kufanya vizuri kwenye michezo.