Jumatatu , 7th Nov , 2016

Barcelona imesherehekea kilele kingine cha mafanikio cha Lionel Messi baada mshambuliaji huyo wa Argentina kufunga goli la 500, kwa klabu yake, usiku wa jana.

Lionel Messi

 

Messi mwenye umri wa miaka 29, alifunga bao la kwanza wakati Barcelona ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Sevilla, uwanja wa Estadio R. Sanchez Pizjuan.

Messi anafikisha idadi hiyo, ya mabao katika michezo 592, ukijumuisha na michezo ya kirafiki ya klabu hiyo ya Catalunya, huku 469, ikiwa michezo ya mashindano.

Messi, amemzidi mabao 105, mfungaji namba mbili wa muda wote wa klabu hiyo, Paulino Alcantara, aliyechezea kipindi cha mwaka 1912 na 1927.