Jumatano , 14th Sep , 2016

Meneja wa mchezaji wa Simba Mohamed Hussein Tshabalala Henry Mzozo amemshukuru mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu ya Simba, Zacharia Hans Pope kwa kutimiza ahadi yake ya kumkabidhi gari mchezaji huyo baada ya kuridhishwa na kiwango chake.

Hanspope (KUlia) akimkabidhi Tshabalala zawadi ya gari

Mzozo amesema kwamba Hans Pope amefanya jambo jema ambalo linafaa kupongezwa hasa baada ya kutambua mchango wa mchezaji kwa kuwa jambo hilo litampa faraja kubwa mchezaji mwenyewe na kuendelea kuitumikia vyema timu ya Simba.

Amesema kwamba mbali na kumkabidhi gari, pia amempa shilingi milioni moja fedha za Tanzania kwa ajili ya kumsaidia kununua mafuta ya gari hiyo.