Jumatatu , 23rd Nov , 2015

Kocha msaidizi wa timu ya JKT Ruvu, Mrage Kabange amesema wanaamini mechi za kirafiki ni mwalimu mzuri wa kuweza kukiweka kikosi vizuri kwa ajili ya michuano ya ligi kuu ya soka Tanzania Bara.

Kabange amesema, wanajaribu kutafuta mechi za kirafiki za nguvu ili ziweze kuwasaidia kuimarisha kabisa kikosi chake.

Kabange amesema, "Unapopata mechi za kirafiki zinakupa mwelekeo kama kikosi chako kipo tayari au bado na zinakusaidia kuweza kutambua ni kitu gani unatakiwa kuongeza au kuboresha katika kikosi chako".

Kabange amesema, kwa sasa anawajenga mwili wachezaji wake ili kuwa katika hali nzuri ya kimchezo na kuweza kufanya vizuri ili kutoka katika nafasi waliyopo hivi sasa.