Ijumaa , 23rd Jan , 2015

KIKOSI cha wachezaji 14 na viongozi watatu kutoka Zanzibar kimewasili jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuunda kambi ya timu ya Taifa ya mpira wa Ufukweni ambapo wanatarajia kuungana na timu ya Taifa ya Mpira wa Ufukweni ya Tanzania Bara.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka nchini TFF,
Boniface Wambura amesema, timu zitacheza zenyewe kwa kushindana ambapo zitatoa fursa kwa benchi la Ufundi kuweza kuchagua timu ya mwisho ambayo itacheza mechi ya mzunguko wa kwanza na timu ya Kenya itakayochezwa Mombasa nchini humo kati ya Febriari 13 na 15 mwaka huu kwa ajili ya Fainali za Afrika zinazotarajiwa kufanyika April Mwaka huu Shelisheli.

Wambura amesema, timu za Tanzania na Zanzibar zitaanza michuano ya mchujo hapo kesho na kumalizika Januari 25 ambapo baada ya hapo itakuwa imepatikana timu kamili itakayoweza kushiriki mashindano hayo.