Meneja Usajili wa Mbeya City FC, Frank Michael Mfundo amesema, Mbeya City bado inashughulikia usajili wa mchezaji mwingine mpya, kabla ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara Desemba 15, mwaka huu.
Mfundo amesema, kocha amependekeza nafasi ya wachezaji watano, tayari wamekwishakamilisha wanne na wakati wowote watamtangaza mchezaji wa kukamilisha idadi ya wapya hao watano waliopendekezwa na mwalimu.
Katika kuendelea kujiimarisha zaidi, kikosi cha Mbeya City FC leo kitakuwa Makambako kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Njombe Mji ya Njombe inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara, ikiwa ni maandalizi kwa Mbeya City kujiandaa na na mechi dhidi ya Mtibwa Sugar Jumamosi.