Jumanne , 31st Mei , 2016

Kocha Roy Hodgson ametaja kikosi chake cha wachezaji 23 wa timu ya taifa ya Uingereza huku mchezaji kijana wa Manchester United, Marcus Rashford, akijumuishwa katika kikosi hicho kitakachocheza michuano ya Mabingwa wa Ulaya, Euro 2016.

Marcus Rashord akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kuifungia Uingereza goli.

Marcus Rashford, mwenye umri wa miaka 18, alifunga goli lake la kwanza akiichezea timu ya taifa Uingereza kwenye mchezo wa Kimataifa wa kirafiki walioshinda kwa magoli 2-1 dhidi ya Australia siku ya Ijumaa.

Mshambuliaji wa timu ya Liverpool Daniel Sturridge ameorodheshwa kwenye kikosi hicho, hata hivyo mchezaji wa Newcastle United Andros Townsend na Danny Drinkwater wa Leicester City wameachwa.

Kikosi chote cha Uingereza kilichotangazwa na kocha Roy Hogson ni kama ifuatavyo:-

Makipa: Joe Hart (Manchester City), Fraser Forster (Southampton), Tom Heaton (Burnley).

Mabeki: Gary Cahill (Chelsea), Chris Smalling (Manchester United), John Stones (Everton), Kyle Walker (Tottenham Hotspur), Ryan Bertrand (Southampton), Danny Rose (Tottenham Hotspur), Nathaniel Clyne (Liverpool).

Viungo: Dele Alli (Tottenham Hotspur), Ross Barkley (Everton), Eric Dier (Tottenham Hotspur), Jordan Henderson (Liverpool), Adam Lallana (Liverpool), James Milner (Liverpool), Raheem Sterling (Manchester City), Jack Wilshere (Arsenal).

Washambuliaji: Wayne Rooney (Manchester United), Harry Kane (Tottenham Hotspur), Jamie Vardy (Leicester City), Daniel Sturridge (Liverpool), Marcus Rashford (Manchester United).