
Haji Manara akisalimiana na Meneja wa Power Dynamos ya Zambia
Manara amesema umaarufu huo umetokana na kiungo wa klabu hiyo aliyesajiliwa msimu huu, Clatous Chama ambaye ni raia wa Zambia. Video inayomuonesha Haji Manara akimtambulisha mchezaji huyo ilisambaa nchini Zambia kiasi cha kumpa umaarufu mkubwa ambao ameushuhudia.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara ameandika, "‘clip yako uliyokuwa ukimtambulisha Clatous Chama imekuwa maarufu sana hapa Zambia’..... Maneno ya Meneja wa Power Dynamos ya Zambia kwangu jana jioni tulipokutana Kwenye mazoezi ya Bingwa wa kihistoria wa Afrika Mashariki na kati Simba, yaliyofanyika katika viwanja vya miamba hiyo ya Zambia".
Simba ipo nchini Zambia kwaajili ya mchezo wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Nkana Red Devils Jumamosi, Disemba 15.
Katika mchezo huo, Simba inatafuta nafasi ya kuingia hatua ya makundi ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza baada ya miaka kadhaa.