
Jose Mourinho (kushoto) na Mwana FA (kulia)
Mourinho ambaye amekuwa kocha wa Tottenham hivi karibuni, anakwenda kukutana na timu ya Man United ambayo aliifundisha kutoka mwaka 2016 hadi 2018, alipofutwa kazi kutokana na matokeo mabovu.
Tangu ameichukua Tottenham, tayari ameshashinda mechi mbili za Ligi Kuu pamoja na moja Ligi ya Mabingwa. Alicheza na West Ham akashinda 3-2, akashinda 3-2 dhidi ya Bournemouth, kisha 4-2 dhidi ya Olimpiakos.
Shabiki mkubwa wa Man United hapa nchini, msanii Mwana FA amemuomba Mourinho awasaidie kumfukuzisha kazi kocha wao Ole Gunnar Solskjær.
'Leo ndio ile siku mwanangu mwenyewe Mreno sio? kwa hiyo tunafanyaje? utusaidie kumng’oa Babyface ili Poch apewe timu yake ama utupe points tujikongoje, chaguo lako', ameandika Mwana FA.
Katika mechi tano za mwisho ilizocheza Man United kwenye ligi kuu pamoja na Europa League, imeshinda 2, kufunga 1 na sare 2.