Akizungumza na East Africa Radio, aliyekuwa mchezaji wa Klabu ya Simba B ambaye amesajiliwa na Klabu ya Neckarsulmer Union Sports inayoshiriki liki kuu ya Ujerumani maarufu kama Verpansliga nchini Ujerumani, Emily Mgeta amesema, nchi nyingi duniani kauli mbiu ni kuwekeza kwa vijana kwa kujua wanaochipukia wanakuwa na misingi bora ya kisoka.
Kwa upande, mwingine Emily amewataka mashabiki wa soka hususani timu ya Taifa hapa nchini kuacha kutoa lawama kwa timu inapofanya vibaya na inatakiwa kuipa timu matumaini kwani inapofanya vibaya leo wajue wanajipanga kwa kesho na kwa kufanya hivyo itasaidia Tanzania kufika mbali zaidi katika soka.