Maguri ameachwa na Simba kwa madai kuwa kocha Dylan Kerr ameonesha kutoridhishwa na kiwango chake.
Maguri aliyesajiliwa na Simba msimu uliopita akitokea Ruvu Shooting kwa mkataba wa miaka miwili aliachwa na kocha Kerr katika kikosi kilichokuwa kikijiandaa kupambana na Sports Club Villa ya Uganda August nane mwaka huu huku ikisemekana kuwa Simba imeamua kuachana na mshambuliaji huyo na anaweza kupelekwa kwa mkopo au akauzwa kabisa.

