Kocha wa timu hiyo Valentina Quaranta amesema anaamini kikosi chake chenye wachezaji 17 kinachotarajia kushuka dimbani leo kuikabili Zimbabwe mchezo utakaochezwa katika uwanja uliopo Johannesburg nchini Afrika Kusini kitafanya vizuri na kuweza kuendelea mbele na hatimaye kufanikiwa kushiriki michuano ya olimpiki.
Timu za wanawake zinazoshiriki michuano hiyo ya kuwania nafasi ya kufuzu kushiriki michuano ya Olimpiki Rio 2016 Ghana, Nigeria, Tanzania, Kenya, Zimbabwe na Namibia.