
Messi amechukua uamuzi huo wakati timu ya soka ya taifa ya Argentina ikiwa imepoteza ushindi mara nne katika miaka tisa kwenye michuano mikubwa ya kimataifa.
Mchezaji huyo amesema kwake yeye basi tena hatochezea timu ya taifa, na kuongeza kuwa amefanya kila awezalo na inauma sana kutokuwa bingwa wa Copa America.
Katika klabu yake ya Barcelona, Messi ameshinda ubingwa wa ligi ya Hispania La Liga mara nane na Ligi ya Mabingwa wa Ulaya mara nne. Kwa timu ya taifa Messi alishinda medali ya dhahabu katika Olimpiki mwaka 2008.