Jumatano , 11th Aug , 2021

Baada ya siku ya jana klabu ya PSG kumsajili Lionel Messi, sasa anatajwa kuwa ndiye mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi klabuni hapo huku kwa mwaka akiwa anavuta Euro zaidi ya Milioni 35 ambazo ni sawa na Tsh. Bilioni 95.

Picha na Mchezaji Lionel Messi

Rafiki yake Neymar anafuatia kwa mshahara wa Euro Milioni 30 ambazo ni sawa na Tsh. Bilioni 81.3 kwa mwaka huku mfaransa Kylian Mbappé akilamba Euro Milioni 24 amabzo ni sawa na Bilioni 65.1 kwa mwaka.

Messi ataitumikia PSG mpaka 2023 akiwa klabuni hapo na rafiki yake Neymar ambaye ameungana nae tena baada ya kucheza pamoja huko Barca.