Jumapili , 3rd Mei , 2015

Ligi ya wilaya ya Dodoma hatua ya sita bora inatarajiwa kuanza kutimua vimbi hapo kesho uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Katibu wa Chama cha Soka cha Wilaya ya Dodoma Mjini DUFA, Ramadhan Panga amesema ligi hiyo inaanza baada ya hatua ya makundi kukamilika ambapo timu sita zimefanikiwa kufika hatua hiyo.

Panga amesema, timu zilizofanikiwa kufika hatua hiyo ni Nkuhungu, Nkulabi FC, Angastone FC, Young Stone FC, Pentagon na Veyula.