Ijumaa , 23rd Jan , 2015

Michuano ya Ligi kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea hapo kesho ambapo timu ya Yanga itakuwa ugenini na Polisi Morogoro mechi itakayochezwa uwanja Jamhuri mjini humo.

Katika muendelezo wa michuano hiyo, Jumapili kutakuwa na mechi kadhaa ambapo zitawakutanisha Azam na Simba mechi itakayochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaa, huku Kagera Sugar ikiikaribisha Ndanda uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, Coastal Union ikikaribisha na Stand United Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, Mbeya City ikikutana na Tanzania Prisons uwanja wa Sokoine Mbeya, Ruvu Shooting na Mtibwa Sugar ambao watakutana uwanja wa Mabatini Mlandizi na JKT Ruvu watakutana na Mgambo Shooting uwanja wa Chamazi jijini Dar es salaam.

Wambura amesema, katika michuano hiyo ya Ligi kuu, kulitokea vurugu katika mechi zilizopita ambapo Yanga walikutana na Ruvu Shooting na kutokea vurugu katika mechi hiyo ambapo amewaomba Yanga kuzingatia taratibu na sheria za Soka ili kuweza kupata haki kwani hakuna Sheria inayoruhusu taarifa ya msimamizi kutolewa hadharani.