
Kiungo wa Liverpool, Georginio Wijnaldum kwenye moja ya mchezo wa EPL.
Wijnaldum kiungo Mholanzi ambaye amepata mafanikio makubwa na klabu ya Liverpool, amegoma kuongeza mkataba mpya wa kuendelea kuwepo klabuni hapo, licha ya kuhitajika katika mipango ya kocha Jurgen Klopp.
KWANINI ANATAKA KUONDOKA?
Wadadisi wa mambo wanaona kama ni njia ya kumkimbia kiungo mpya katika timu hiyo, Thiago Alcantara aliyejiunga kutokea Bayern Munich katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi.
Wijnaldum amekuwa akihusishwa na kujiunga na Barcelona tangu Mholanzi mwenzake Ronald Koeman achukue jukumu la kuifundisha timu hiyo.
Ujio wa Thiago Alcantara umezua hofu kwa baadhi ya wachezaji wa liverpool, kutokana na umahri wake wa kuchezesha timu, kupiga pasi za uhakika, ubunifu wa hali ya juu na usahihi wa matendo yake mchezoni, ukifananisha na viungo wengine wote wa liverpool akiwemo Wijnaldum
Wijnaldum ambaye amecheza michezo 189 tangu ajiunge na klabu hiyo mwaka 2016 akitokea Newcastle ambapo ameshiriki ipasavyo katika mafanikio ya liverpool kwenye kutwaa ubingwa wa ligi ya mabingwa Ulaya, ubingwa wa ligi kuu England na ubingwa wa kombe la Dunia la FIFA kwa ngazi ya vilabu 2019