
Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire akizungumza jambo ndani ya Studio za East Africa Radio.
Masau amesema ''hata kama uwanja una kasoro lakini kanuni zinaelekeza kutoa muda wa siku 21 kwa timu husika kutafuta uwanja mwingine wa kuchezea jambo ambalo bodi ya ligi wamelikiuka kwani wao wanamchezo dhidi ya Biashara siku ya jumapili''
“Kama ukifuatilia sisi pale uwanjani kwetu tuna vyoo maeneo mawili, tunavyoo upande wa kusini mashariki, vyoo vile vina matundu manne lakini pia tuna choo upande wa kaskazini magharibi ambacho kina mashimo manne, tunavyoo ambavyo huwa vinatumika kwa ajili ya watazamaji ambao wapo jukwaa kuu vya kisasa kabisa ambavyo huwa vinatumika, sasa ukisema hakuna vyoo vya kutosheleza sijajua unafanya mahesabu gani” Alisema Masau Bwire
Vile vile Bwire anasema katika kasoro ya vyoo ambayo bodi wameiainisha haiko sahihi kwasababu katika uwanja wao una vyoo vya kisasa ambavyo pia vinatumika.
Kwa sasa Ruvu itatumia uwanja wa uhuru katika mchezo wa Jumapili.