Kocha wa timu za Taifa za Kriketi Wanawake na Wanaume Hamisi Abdalah amesema mikoa ya kriketi ya Dar es Salaam, Morogoro, Arusha na Tanga wataanzisha kambi zao kwa ajili ya kupata timu zao zitakazo pambanishwa mwezi machi mwaka huu ili kupata timu moja ya Taifa.
Abdala amesema kwa sasa programu hiyo inaanzia kwa sehemu walipo wachezaji kwa vile wengi wao ni wanafunzi na wakifunga shule kutakuwa na kambi ya pamoja itakayokuwa Dar es Salaam na kubaki na wachezaji 14 kutoka wachezaji 20 watakaoenda Afrika Kusini.

