Ijumaa , 12th Feb , 2016

Kozi ya makocha wa kuogelea inatarajiwa kuanza Februari 15 mwaka huu jijini Dar es salaam kwa kushirikisha makocha takribani 50 kutoka hapa nchini.

Katibu Mkuu wa TSA Ramadhan Namkoveka amesema kozi hiyo itakuwa ya siku tano ambapo mpaka sasa wana washiriki 35 ambao wamekwishajiandikisha kwa ajili ya ushiriki wa kozi hiyo.

Namkoveka amesema, uandikishaji wa washiriki wa kozi hiyo unatarajiwa kufungwa hapo kesho ambapo wanatarajia kuwa na makocha 50 ambao watapokea mafunzo kutoka kwa mkufunzi kutoka nchini Marekani.

Namkoveka amesema, mkufunzi huyo anatarajiwa kuwasili siku ya Jumapili kwa ajili ya kuanza kazi hiyo ya kufundisha makocha na waogeleaji mbinu mbalimbali za kuwawezesha kufanya vizuri katika mchezo huo.