
Kocha Morocco amesema kila kitu kilikwenda vizuri kuhusiana na kusaini mkataba kuanzia akiwa Zanzibar, hadi alipofika jijini Dar es Salaam, lakini ghafla anashangaa rais wa Simba kubadilika.
Morocco amesema alishapata nakala kutoka TFF inayomruhusu kuifundisha Simba na alikuwa tayari kufanya nao kazi lakini makubaliano ya kimkataba waliyokubaliana yamekuwa kinyume.
Hivi karibuni, Morocco alipewa jukumu la kuwa kocha msaidizi wa Taifa Stars, akisaidiana na Boniface Mkwasa kama kocha mkuu kabla ya Simba kumfuata na kumpa kibarua cha kukinoa kikosi hicho.
Hiyo ni siku chache tangu ifahamike kuwa kocha huyo wa Mafunzo ya Zanzibar, huenda akasaini mkataba wa miezi sita wa kuwa mkurugenzi mkuu chini ya Mganda, Jackson Mayanja.