Jumamosi , 19th Feb , 2022

Licha ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Torino kwenye mchezo wa Ligi Kuu Italia Serie A’ jana usiku kocha wa Juventus Massimiliano Allegri amewasifu wachezaji wake kwa kupambana na anaamini timu inabadilika kadrid siku zinavyokwenda na wanaelekea sehemu nzuri.

Kocha wa Juventus Max Allegri

Kibibi kizee cha Turin Juve ndio walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 13 kupitia kwa Matthijs de Ligt kabla ya Andrea Belloti kuisawazishia Torino kipindi cha pili dakika 62 ya mchezo huo ambao Juventus walikuwa wenyeji katika dimba la Allianz.

Kwa upande wa Kocha Max Allegri alionyesha kuridhika na kiwango cha uchezaji cha timu yake licha ya sare ya pili mfululizo,

"Kwa kushangaza, tuliruhusu bao katika nyakati ambazo tulikuwa bora zaidi. Katika kipindi cha kwanza tulikuwa na nafasi mbili au tatu ambazo tungeweza kufunga, lakini sio kipindi cha pili. Kipindi cha pili hatukuwa vizuri sana, lakini nadhani ni hali ya kawaida, ni jambo la kawaida unapocheza kwenye ligi, haswa unapolenga kuingia kwenye nafasi nne za juu , kwa hivyo sare sio ya kuibeza. vijana wamecheza mchezo mzuri wamejituma na wamecheza kwa nguvu. Walipambana kuhakikisha wansahinda hadi dakika za mwisho.” Amesema Allegri

Hii ni sare ya pili mfululiz na kwenye michezo ya Ligi Kuu Serie A nay a 5 katika michezo 5 iliyopita, kwani kabal ya mchezo huu dhidi ya Torino walitoka sare ya bao 1-1 na Atalanta. Kwa matokeo haya Juventus imefikisha alama 47 wakiwa nafasi ya 4 kwenye msimamo wa Ligi tofauti ya alama 8 dhidi ya AC Milan ambao ndio vinara wakiwa na alama 55.